WAZIRI WA ELIMU AKERWA NA DARAJA LA TANO KUITWA SIFURI



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ameelezea kukerwa na daraja la tano katika muundo mpya wa kupanga matokeo, kuitwa sifuri.
 
Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
 
Alivishutumu vyombo vya habari kwa kuchanganya alama na madaraja yaliyopo katika muundo mpya wa kupanga matokeo ya mitihani nchini.
 
Alisema kwa muundo mpya, daraja sifuri ni kati ya pointi 48 na 49 ambayo inapatikana baada ya mtahiniwa kupata alama F kwa masomo yote saba.
 
“Ndugu zangu waandishi wa habari, kitu ambacho hamkufanya haki kwa Watanzania safari hii, ni ile kuliita daraja la tano kuwa ni sifuri mkalazimisha na mimi kumwagiza Katibu Mkuu abadilishe na kuita daraja sifuri,” alisema na kuongeza:
 
“Unakuaje na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne lakini unapofika la tano unaita sifuri katika namna ambavyo waandishi wa habari walipenda.”
 
Dk Kawambwa alisema vyombo vya habari vimekuwa vikipenda taswira ya nchi ionekane kuwa ni kufeli. “Lakini ninachosema ni kwamba, pointi ni zile zile tulichoondoa ni daraja la tano.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo