Daktari: Jana Membe aliletwa hospitali tukamtibu na kumruhusu


Akizungumza leo Mei 12,2023 majira ya asubuhi, Daktari wa Hospitali ya Kairuki ambako Membe alifikishwa kwa matibabu Dk.Asseri Mchomvu amesema walimpokea Membe saa 12:30 akiwa na changamoto ya upumuaji na hivyo jopo la madaktari wakaanza kumpatia matibabu lakini baadae akaaga dunia.


Ameeleza kuwa kabla kufariki Dunia jana Membe alifikishwa katika hospitali hiyo ambako alipatiwa matibabu na kuruhusiwa lakini leo alirudishwa tena baada ya kuzidiwa kwa changamoto ya upumuaji.

Dk.Mchomvu alipoulizwa changamoto ya Membe ilikuwa ni nini?Amejibu kwa kifupi kwamba alikuwa anasumbuliwa na upumuaji na ndio ambao madaktari walikuwa wakipambana kuokoa uhai wake lakini ikashindana na kufikwa na umauti.

Hata hivyo taarifa za kifo hicho zimeendelea kusambaa maeneo mbalimbali nchini na hiyo inatokana na umaarufu aliokuwa nao Membe enzi za uhai wake lakini katika mitandao ya kijamii nako kumeibuka maswali mengi kuhusi kifo chake kutokana na sababu mbalimbali (Tumezihifadhi)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo