Mtumiaji mmoja wa mtandao uitwao Douyin ambao ni toleo la Tik Tok nchini China amefariki dunia baada ya kudaiwa kunywa pombe kupita kiasi.
Vyombo vya habari vya China vimeripoti kuwa mtu huyo alikutwa amefariki dunia saa 12 baada ya programu yake katika mtandao huo.
Kifo chake kilichojadiliwa sana kwenye mtandao huo wa Douyin, kimeibua vuguvugu la kutaka kuwepo kwa kanuni kali za tasnia inayokua inahusika na programu hizo.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye ametambuluwa kwa jina la Wang, alikua amebobea katika kunywa aina ya pombe iliyotengenezwa nchini China yenye kilevi cha asilimia 60.
Rafiki yake amekiambia chombo Cha habari Cha china kuwa kijana huyo alimaliza programu yake majira ya saa sita usiku na kufariki siku iliyofuata, na bahati mbaya familia yake haikufanikiwa kumuokoa kwani walikuta kashafariki
Kijana huyo alikua amebobea katika michezo ambapo alishiriki mapambano manne na kushindwa matatu na akapewa adhabu ya kunywa chupa za baiju na inasemekana alikunywa hadi angalau chupa saba, na haikuishia hapo kijana huyo alikua ameshaonywa awali kwa progamu yake hiyo ya kunywa pombe lakini alikwepa na akaamua kufungua akaunti mpya