Waiachia Serikali imzike ndugu yao Baada ya Kushindwa Kulipa Bili ya Hospitali


Familia moja kutoka kaunti ya Kiambu imetaka hospitali kuuzika mwili wa mpendwa wao baada ya kushindwa kupata kiwango cha fedha walizokuwa wakidaiwa kama bili ya hospitali.


Familia hiyo iliyoko Kabete inadaiwa bili ya shilingi takribani milioni moja ili kuruhusiwa kuuchukuwa mwili wa mpendwa wao japo wao wanasema kuwa wamejaliwa kupata 40,000 kupitia michango waliofanya. 


Marehehemu aliyefahamika kama Leston Kinuthia alifariki mwezi mmoja uliopita na familia imekosa kupata kiwango kinachohitajika kuutoa mwili wake hospitalini. 


Kulingana na babake Kinuthia Tilas Wangati ambaye amesema kuwa hana njia yoyote ya kulipa bili hiyo ya hospitali amedokeza kuwa waliwasilisha shilingi 40,000 walizopata katika hosptila ili wauchukue mwili wa marehemu lakini hospitali ikadinda kuwapa mpendwa wao kabla hawajakamilisha bili iliyohitajika.


"Nilipatiwa bili ya shilingi 945,000 na nikaona siwezi kulipa hiyo kwa sababu sina kazi sina kitu ambacho ninaweza kuuza. Kwa hivyo nimekata kauli mimi na watoto wangu tunauliza serikali inaweza kutusaidia wazike huyo mtoto wangu," Wangati ambaye ni babake marehemu alisema. 


Dadake Marehemu Rosebel Wairimu amesema kuwa ombi lao la kutaka kumzika mpendwa wao halikuwezekana kwani hospitali ilihitaji angalau thuluthi tatu ya pesa ambazo walikuwa wanadaiwa. 


"Tulitafuta pesa na tukajaliwa kupata 40,000 ambayo haikutusaidia. Tulivyoenda huko kuomba watusaidie walituambia hawawezi na kuwa tulihitajika kutoa angalau thuluthi tatu ya pesa na kisha twende na kitu kitakachoonyesha kuwa tutakamilisha kulipa salio," Wairimu alisema. Familia imesema kuwa kwa sasa hawana namna ya kutoa mpendwa wao kutoka hospitalini humo na kuwa wanaisihi hospitali kuwasaidia kumzika mpendwa wao.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo