Baadhi ya waliopora mali katika shamba la familia ya Kenyatta la Northlands Kiambu kaunti wamerejesha walichoiba.
Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Nation, baadhi ya mifugo ambao waliibwa wakati genge la vijana lilivamia shamba hilo Machi 27,2023 wamerejeshwa.
Gazeti hilo linasema polisi wameripoti kuwa kondoo kumi na wanane waliokuwa wameibwa walirejeshwa. Ripoti zinasema wandani wa wanasiasa fulani wamekuwa wakirudisha kondoo hao usiku na kuwaweka karibu na shamba hilo.
"Ni kweli tumeweza kupokea kondoo 18 na tunaamini wote watarejeshwa," meneja wa shamba hilo Patrick Masinde alisema.
Chanzo: TUKO.co.ke
