Waliokuwa wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wametangaza kujiunga na Chadema ikiwaa ni siku chache tangu walipotangaza kujivua uwanachama wa chama hicho.
Februari 23 mwaka huu wanachama wa CUF zaidi ya 384, walitangaza kujivua uanachama kwa kile walichodai chama hicho kimepoteza mwelekeo, huku wakimtuhumu Mwenyekiti Profesa Ibrahimu Lipumba kukiuka katiba ya chama hicho.
Wanachama hao wametangaza uamuzi huo leo Jumamosi Machi 11, 2023 katika Ukumbi wa Garden uliopo Kinondoni.
Katibu wa kamati hiyo, Shahada Issa amesema walifanya uamuzi wa kujivua uanachama wa CUF kutokana na chama hicho kukosa muelekeo.
Amesema walizungumza na vyama mbalimbali na baada ya kutafakari kwa kina wwliona ni vyema kujiunga na Chadema ili kusongesha gurudumu kuelekea 2025.
Amesema baada ya kufanya uamuzi huo wanatarajia kuanza kuzunguka maeneo mbalimbali ili kujenga na kuendelea kukiimarisha chama hicho.
Baada ya kutangaza kujiunga na Chadema wanaelekea makao makuu ya chama hicho kwaajili ya kukabidhiwa kadi.