Neema Cheyo mkazi wa tarafa ya Bukene wilayani Nzega mkoani Tabora, amepoteza maisha baada ya mzazi mwenzake kumkata na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni panga katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani mwanaume huyo alikuwa anang'ang'ania kuendelea na mahusiano hao licha ya wao kuachana.
"Tukio hilo limetokea Februari 21, 2023, majira ya saa 2:00 usiku ambapo baada ya kujeruhiwa na mzazi mwenzake alikimbizwa hospitali ya Nzega ambapo hali yake ilikuwa mbaya na alipoteza maisha, chanzo ni wivu wa mapenzi, Neema alikuwa hataki kurudiana na mwanaume wake wa zamani na alimpa lakini nne ili mahusiano yavunjike lakini mwanaume huyo hakuridhika," amesema Kamanda Abwao.
Kamanda Abwao amesema kwamba mwanaume aliyehusika na mauaji hayo amekamatwa na atafikishwa mahakamani.
Chanzo:EATV