Mwanaume ukitelekeza mtoto jela miezi 6, faini Tsh mil 5

Afisa Ustawi wa jamii katika halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Rosemary Wilfred amesema sheria ya sasa kwa mwanaume anayetelekeza mtoto baada ya kuzaa na mwanamke inamtaka mwanaume kulipa faini ya Tsh milioni 5, ama kufungwa jela miezi sita au kutumika adhabu zote kwa pamoja.


Akizungumzia hilo, Afisa huyo wa ustawi wa jamii Jiji la Dar es salaam amesema tatizo la utekelezaji watoto kwa mkoa wa Dar es salaam ni kubwa kwani Kwa wastani kwa siku wanapokea kesi 15 za watoto kutelejezwa na baba zao.

Amesema wao kama maafisa wa ustawi wa jamii wanaendelea kuelimisha jamii juu ya kuzifahamu sheria za makuzi na malezi ya mtoto Ili kulinda haki za mtoto za kupata malezi kutoka pande zote mbili za wazazi.

Nao wananchi wa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam wakiwemo waliotelekezewa watoto na wanaume zao wameitaka serikali kusimamia sheria hiyo kwa kuwa kama utekeleza ji wake utafanyika wanaume wengi wataacha tabia hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo