Mbunge wa CCM amshukia vikali Dkt. Slaa, adai amepoteza mwelekeo

MBUNGE wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu amejibu aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk.Wilbroad Slaa kuwa amepoteza mwelekeo baada kukosa nafasi serikalini.


Dk.Slaa hivi karibuni ameibuka kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) wilayani Karatu akitoa maneno ya kukikashfu Chama Cha Mapinduzi(CCM) huku akisema katiba mpya isiwe na Wakuu wa Wilaya.

Kutokana na kauli hizo alizotoa kwenye mkutano wa Chadema, Mtaturu amesema ni vyema Dk.Slaa kuwa mzee mwenye busara baada ya kukosa nafasi.

Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, Mbunge huyo amesema kuna umuhimu wa Wakuu wa Wilaya kuendelea kuwepo kwenye katiba kutokana na umuhimu wao katika kusimamia maendeleo ya wilaya.

Amesema kwa sasa watanzania wanataka kusikiliza hoja zenye mashiko na maendeleo.

“Hapa jimboni nilipoingia tulikuwa nyuma kimaendeleo tangu mwaka 2018 hadi sasa hakuna kata wala kijiji kisicho na mradi wa shule, na kwamba hali hiyo imeongeza imani kwa wananchi,”amesema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo