Mke Amtafutia Mumewe Mchepuko ili aache Uzinzi

Mwanamke kutoka Long Island nchini Marekani, amemtambulisha mwanamke mwingine ambaye anafanana naye katika ndoa yake yenye doa ili kumzuia mume wake mzinzi kuwanyemelea wanawake wengine.


Kulingana na New York Post, Tehmeena Quintana alikerwa sana wakati mume wake Bryant Quintana alipochepuka miaka mitatu baada yao kuoana na hivyo aliwazia kutatua matatizo yao kwa kujaribu ndoa ya wazi. 


Kulingana na mke aliyejitolea, Bryant hakuwa mwaminifu kwake hapo zamani pia. "Ninahisi kwamba ikiwa uko na mwanamume, unapaswa kufanya chochote kinachohitajika kusimamisha ndoa yakeo," alisema.


“Nataka kuishi maisha yangu yote naye. Chochote anachotaka, chochote kinachomfurahisha, nitampa," aliongeza. Tehmeena aliamua kutumia mitandao ya kijamii kumtafuta mtu anayefanana naye ili kuingia katika ndoa ya mtaala. Tangu wakati huo alikiri kwamba alihisi kutokuwa salama alipotafuta mtu wa tatu kuwa katika uhusiano wao. "Nilijua kwamba ingeweka akili za Bryant hapa. Ni sawa kusema nilitafuta msichana anayefanana nami kwa sababu Bryant anapenda hivyo," alisema. 


Hatimaye, Tehmeena alipatana na mwanamitindo wa Australia Kyrah Johnson, ambaye kwa muonekano anafanana naye kama shillingi kwa ya pili. Warembo wote wawili wana matiti makubwa, na kope laini. Kyrah alisafiri kwa ndege hadi New York kukutana na Tehmeena na Bryant akisema kutokea kuwa marafiki sasa wanalala kitanda kimoja pamoja. 


Kyrah amesema kuwa anapenda jinsi anavyofanana na Tehmeena. "Tunapoenda nje kila mara tunaulizwa kama sisi ni dada au mapacha!" alisema. 

Chanzo:tuko.co.ke


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo