Katika kisa kilichotokea mtaani Dagorreti huko nchini Kenya, mwanamke mwenye umri wa miaka 26, ambaye anatumikia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuwaua watoto wake wawili alisimulia kilichotokea siku hiyo ya mauti.
Diana Kibisi aliua watoto wake wa miaka minne na miaka miwili eneo la Waithaka, Dagoretti, Nairobi na baadaye kujisalimisha kwa kituo cha polisi ambapo alikiri kufanya uhalifu huo.
Akizungumza katika mahojiano na Inooro TV, mwanamke huyo ambaye alisema anajutia kufanya unyama huo, alikumbuka kuwa mama yake na shemeji yake walimtembelea siku hiyo hiyo ambayo watoto wake walikufa mnamo 2021.
Chanzo:tuko.co.ke