Kundi la wanamgambo wa Boko Haram limesema kuwa limebuni taifa la kiislamu katika miji na vitongoji inavyotawala kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji
wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.
Haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa
wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu
kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.
''Ningependa kuwashukuru sana ndugu zetu ambao wamefanikiwa kukomboa ardhi na nyoyo za watu huko Iraq na Syria'' alisema bwana Shekau japo haikubainika iwapo ni wa moja au la.
''Nashukuru Allah kwa ndugu zetu waliokomboa mji wa Gwoza na
wakaufanya kuwa sehemu ya himaya ya Islamic state,"alisema bwana
Shekau katika ukanda huo wa videowenye urefu wa dakika.
Jeshi la Nigeria limepuuza dai hilo kuwa “tupu.”
Jeshi la Nigeria limepuuza dai hilo kuwa “tupu.”
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade
alipinga tangazo hilo akisema kuwa ''Hakuna hata nchi moja ya taifa hilo
iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni moja.''
Maelfu ya watu wameuwawa kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu 2009, wakati Boko Haram ilipoanza uasi wake.
Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.
Chanzo:BBC
Chanzo:BBC
