Binti Afungwa Jela Miaka 10 kwa Kumtumia Bosi Wake Picha za Utupu Kimakosa

Mwanamke kutoka Eldoret nchini Kenya ambaye ana miezi minane katika kifungo chake cha miaka 10 jela katika Gereza la Wanawake la Lang'ata, amesimulia uhalifu uliomsababisha kufungwa jela.


Mercy Chepchumba anatumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kumtumia bosi wake picha za utupu. Akizungumza katika mahojiano na Inooro TV, Chepchumba alieleza kuwa masaibu yake yalianza alipojiunga na kundi la WhatsApp la kutuma picha chafu hivyo katika harakati hiyo alimtumia bosi wake wa kike kimakosa. 


"Nilikuwa nimejiunga na kikundi hiki cha kutuma picha zako binafsi, na kwa namna fulani nilimtumia bosi wangu, ambaye hapo awali aliniajiri nyumbani kwake kama msaidizi wa nyumbani, picha yangu chafu namna hiyo. Alikasirika sana, na pia niliomba msamaha kama vile kadiri nilivyoweza,” alisimulia Chepchumba.


Alisema mambo yalizidi unga alipoamua kumbloki bosi wake akitarajia kutuliza mvutano kati yao, lakini hatua hiyo lilizidisha chumvi kwenye kidonda kwani mwajiri wake alienda kumripoti kwa polisi. “Polisi walinijia Kayole baada ya kufanikiwa kunifuatilia, nimejifunza mambo mengi sana nikiwa humu ndani, kama ningerudishiwa uhuru wangu nisingerudia tena, sikujua kutuma picha za aina hiyo kunaweza kuniweka taabani na sheria," alisema Mercy huku akijutia. Mercy alisema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo na anatumai atashinda kwani tayari amepata funzo kupitia njia ngumu. 


Katika taarifa tofauti, mwanamke Mkenya anayetumikia kifungo cha maisha katika Gereza la Wanawake la Lang'ata, pia alielezea kwa kina mazingira ambayo yalimpelekea yeye pamoja na ndugu zake wengine walifungwa gerezani mwaka wa 2009. Stella Njoki, ambaye amekuwa gerezani tangu 2009, alisema hasira kwa mmoja wa kaka zake ilisababisha kufungwa kwao maisha.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo