Bibi Harusi Atoweka Siku 2 Kabla ya Harusi Akienda Saluni Kujipodoa


Familia moja imeghubikwa na sintofahamu baada ya binti yao kutoweka siku mbili tu kabla ya harusi yake, iliyopangwa kufanyika, Machi 12, 2023.


Najuuka mwenye umri wa miaka 24, alitoweka siku ya Ijumaa, siku mbili tu kabla ya harusi yake ambayo maandalizi yalikuwa yamekamilika. 


Kwa mujibu wa ripoti ya New Vision, Bi harusi huyo alionekana mara ya mwisho katika Jumba la Kibiashara jijini Kampala akiwa na marafiki zake, alikokuwa ameenda kujipodoa. 


Mama yake, Aisha, alisema baada ya kutoka kwenye jumba hilo mwendo wa saa 9 usiku, alikwenda kuabiri teksi kwenye stani ambako kulikuwa na fujo.


Kutokana na hofu kuwa angeharibu vipodozi vyake alivyotengenezwa, aliwaambia marafiki zake kwamba angependelea kuchukua teksi kwenye stani nyingine. Tangu wakati huo,ajulikana aliki na simu zake zimezimwa huku juhudi za kumpata zikiambulia patupu. 


"Tumekuwa tukiwasiliana na bwana harusi na anatuthibitishia kuwa hana taarifa zozote aliko," mama huyo aliyekuwa amehuzunika alisema. Harusi hiyo ilikatishwa jana Jumatatu huku wakwe wakaombwa kusubiri hadi ripoti ya mtu aliyepotea kuwasilishwa. Familia yake inahofia kuwa huenda ametekwa nyara na sasa inaomba msaada wa kumpata.



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo