Mwanafunzi afariki dunia baada ya kupewa adhabu ya kuzunguka Uwanja

Taarifa ni kwamba jeshi la Polisi katika kaunti ya Trans Nzoia huko nchini Kenya wanachunguza kifo cha mwanafunzi mwenye umri wa miaka 12, wa Shule ya Msingi ya Namanjalala baada ya kudaiwa kuadhibiwa na mwalimu wake.


Katika kisa hicho cha Ijumaa, Machi 10, Mike Wanjala aliagizwa na mwalimu wake kuzunguka uwanja wa shule mara 13 kama adhabu ya kuvunja mlingoti wa goli. Hata hivyo, baada ya adhabu hiyo, mwanafunzi huyo wa darasa la tano alianza kutapika damu na kuzirai, Kisha mwalimu anayehusika alimwagiza mlinzi wa shule hiyo kimpeleka mvulana huyo nyumbani.


Kwa bahati mbaya, wazazi wake Wanjala walikuwa wameondoka kuenda kufanya kibarua. Lakini jirani yao ndiye alichukua hatua ya kumkimbiza Wanjala katika Hospitali ya Kaunti ya Kitale. Mama yake, Catherine Wanjala, alifika katika hospitali saa moja baadaye wakati huo mwanawe alikuwa akihudumiwa na madaktari, lakini hali yake ilikuwa mbaya. Kwa bahati mbaya, 


Wanajala alifariki dunia mwendo wa saa tano usiku akihudumiwa na madaktari “Mwanangu alikuwa mzima alipotoka nyumbani kuelekea shuleni asubuhi. Kwa nini mwalimu amwadhibu mtoto hivyo? Inaniuma sana kama mama na nataka haki kwa mwanangu,” alisema Catherine. 


Babake marehemu, Geoffrey Wanjala, alisema alihuzunishwa sana na kifo chake akimuelezea mwanaye kama mtoto mwerevu na tena mwenye nidhamu. "Nimeachwa bila matumaini baada ya tukio hili na hata baada ya kumpoteza mwanangu hakuna mtu kutoka kwa uongozi wa shule aliyekuja hapa kutueleza kilichotokea," alisema Geoffrey. 



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo