Awatoroka polisi wakati akihojiwa


Dereva Bajaji ambaye jina lake halijafahamika anatafutwa na askari polisi baada ya kuwakimbia na kudandia gari la maji katika makutano ya barabara Vigwaza mkoani Pwani wakati akihojiwa kutokana na ajali aliyosababisha ya kumgonga mtu na kumjeruhi.


Dereva huyo alisababisha ajali hiyo katika eneo la Ruvu Darajani na kukimbia lakini alikamatwa baada ya bajaji yake kugonga uzio wa barabara eneo la Vigwaza.

Polisi wanasema mtuhumiwa huyo ametoroka mikononi mwao na kudandia gari la maji na hadi sasa bado hajapatikana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo