Atorokwa na Mumewe kwa Kuzaa Mapacha wenye upofu, Asema ni Laana

Mnamo Novemba 24, 2012, Scovia Nanangwe alikuwa uchungu wa uzazi hivyo aliandamana na mumewe Ronald Irongo hadi hospitalini kujifungua.


Wanandoa hao wakazi wa Kagera Trading Centre, mjini Jinja, Uganda walikuwa wanatarajiwa kupata mtoto mmoja lakini walishtuka madaktari walipowafahamisha kwamba wangepata mapacha. Baada ya saa kadhaa za uchungu wa uzazi, Nanangwe hatimaye alijifungua mapacha wawili wa kiume.


Atemwa na mumewe Hata hivyo, furaha yake ya kuwa mama ilikatizwa ghafla baada ya madaktari kuwapa habari za kuvunja kwambe wavulana hao walikuwa vipofu.


Punde baada ya kupata habari hizo za kusikitisha, mumewe Nanangwe, alimtelekeza hospitali huku akisaidiwa na msamaria mwema kurejea nyumbani. 


Irongo alimkimbia mkewe akisema kutokana na watoto wake wengine kutokuwa na ulemavu wa macho, basi mapacha hao ni wa mwanamume mwingine. Hivyo, aliitelekeza familia yake na kumwacha Nanangwe na mzigo wa kuwalea watoto wao wanane pekee yake. Mapacha hao wanaofanana, Bright Tenywa Irongo na Aman Waiswa Zirimeyi, ambao kwa sasa wana umri wa miaka 10, ni wa tatu katika familia ya watoto wanane. 


“Ilinibidi nitafute njia ya kupata pesa ili kuwalisha na kuwavisha watoto wangu. Hii ilimaanisha kwenda kwenye nyumba za watu kuchimba na kufua nguo zao,” alisema Nanangwe katika mahojiano na Daily Monitor.


Atafuta matibabu Nanangwe alikuwa na matumaini maarifa ya wataalam wa afya kupata suluhu ya wanawe kuweza kuona. Lakini matumaini yake yalizimwa baada ya kuambiwa kuwa upofu wa wavulana hao ni wa kudumu milele kwa sababu hawana retina hali ambayo Nanangwe anasema kwa sasa ameikumbatia na kukubali.


Kwa bahati nzuri, baada ya miaka miwili ya kutengana na mke wake, Irongo hatimaye alirejea nyumbani. Baba huyo wa watoto wanane anasema aliamua kuacha kuwaelezea pacha hao kama laana na kuwakubali kama baraka kwa sababu ya bahati nzuri walizowaletea. Alisema kupitia wanawe, wasamaria wema walijitokeza na kuwasaidia kuwapeleka watoto hao katika Shule ya vipofu ya St Francis katika Jiji la Soroti. Vile vile shughuli zake za kilimo zimepigwa jeki kuwa za kisasa na kuboresha pato lake.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo