Mwanaume mmoja kutoka Kaunti ya Kakamega nchini Kenya David Zakayo, amesema kwamba aliamua kuoa wake 15 kwa sababu yeye ana akili nyingi ambazo haziwezi kubebwa na mke mmoja, ni bora kuwa na wake wengi kuliko kuwa na mpango wa kando (Mchepuko).
Zakayo anao watoto 107 na kwamba wanawake nane ndiyo wanaishi sehemu moja naye huku wengine 7 wakiwa sehemu nyingine na kwamba anawatunza vyema
Mzee Zakayo akizungumza sababu ya yeye kuwa na wake hao 15 na kwamba anaweza kuongeza wengine amesema, "Nimegundua mimi nikiwa na mwanake mmoja na nikiwa na mpango wa kando wawili nitakuwa na hasara zaidi kushinda yule mtu aliyeoa wote hao na kuwaweke wote na hana mchepuko,".
Aidha Mzee Zakayo ameongeza kuwa "Akili yangu haiwezi kubebwa na mwanamke mmoja kwa sababu ni kubwa sana, sasa huwa na-handle ulimwengu mzima kama yai, niko nao 15 na nitaongeza wengine, mimi mali yangu ni akili,".