Afika Kituo cha Polisi na Kuwatukana Askari Kwamba Hawajasoma


Mwanamume amefikishwa mahakamani baada ya kufululiza hadi kituo cha polisi cha Kayole huko Kenya na kuzua usumbufu kwa kuwatukana maafisa wa polisi kuwa hawajasoma.


Mahakama iliambiwa kuwa Peter Mwangi alikuwa ameenda katika kito hicho cha polisi kwa lengo la kumtembelea ndugu yake ambaye alikuwa ametiwa mbaroni. Hakimu Mkuu Francis Kyambia aliambiwa kuwa Mwangi alizua vurugu na kuwatukana maafisa wa polisi katika kituo hicho kuwa hawajasoma. 


"Unashtakiwa kwa kosa la kuzua usumbufu na vurugu katika kituo cha polisi pamoja na kutishia amani kwa kuwatukana maafisa wa polisi kwamba hawajasoma," mshukiwa aliambiwa na Hakimu Kyambia.


Inaarifiwa kuwa licha ya kumiminiwa matusi, maafisa wa polisi walisindikiza Mwangi hadi nje ya kituo hicho ili wao waendelee na kazi huku naye akienda nyumbani. Hata hivyo alitimuka mbio na kurudi kituoni akiwatukana tesa maafisa hao waliokuwa kazini akidunisha kiwango chao cha elimu. “Ndio Mheshimiwa mnamo Machi 3, 2023 niliwatukana maafisa wa polisi katika kituo cha Kayole... 


Ninajutia matendo yangu... Naomba unisamehe sitarudia kosa kama hili tena siku za usoni," Mwangi aliungama makosa yake mahakamani. Mahakama ilimpokeza faini ya shilingi 10,000 au ahudumie kifungo cha miezi sita gerezani.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo