Aangua Kilio Akisimulia Pasta Alivyomfilisi wakati Akitafuta Miujiza

Evarline Okello ambaye anaishi katika mitaa ya mabanda ya Kibera, Nairobi nchini Kenya, ni mwanamke mwenye majuto.


Katika mahojiano na BBC, mama huyo wa watoto wanne alifichua kwamba masaibu yake yalichangiwa na hamu yake ya kutaka kuishi maisha bora. Kulingana naye, alikuwa akihangaika kuwalisha watoto wake aliposikia kwamba kuna pasta mwenye maombi ya nguvu ambaye angemuombea ili apate mafanikio ya kifedha.


Lakini pasta huyo alimtaka apande mbegu ya KSh15,000 ambazo alilazimika kulipa.


Okello alikuwa ameambiwa na aliyemtambulisha kwa mchungaji huyo kuwa maombi yake yalikuwa na nguvu sana kiasi kwamba angeweza kumrudishia pesa yake katika kipindi cha wiki moja. Kulingana na mama huyo, alikopa pesa hizo kutoka kwa rafiki yake, ambaye alichukua mkopo kwa niaba yake Lakini usiku ulikucha bila yeye kuona muujiza na badala yake mambo yalikuwa mabaya zaidi. 


Mkopo ambao rafiki yake alikopa kwa niaba yake sasa umeongezeka hadi kuwa KSh38,000 kutokana na riba ambazo hazikulipwa na swahiba wake pia amegoma kusema naye. "Mambo yamekuwa magumu sana nimepoteza matumaini yote," anasema Okello.


Kanyari Injili ya mafanikio, ambayo inafundisha kwamba Mungu huwazawadia utahiri na afya, umekuwa ukisambaa kote Afrika. Kwa mfano humu nchini, mhubiri tatanishi Victor Kanyari alimulikwa kwa kuibuka tena na njama nyingine ya ‘panda mbegu’ takriban miaka minane tangu kumulikwa na kamera za wanahabari.


Katika kipande cha video kilichozunguka kwenye mitandao ya kijamii, Kanyari anaonekana akiwaambia waumini wake kuwa atamzawadi shilingi 30,000 yeyote atakayetoa sadaka ya shilingi 500. Katika kipande cha video kinachozunguka kwenye mitandao ya kijamii, Kanyari anaonekana akiwaambia waumini wake kuwa atamzawadi shilingi 30,000 yeyote atakayetoa sadaka ya shilingi 500.


Chanzo: BBC na TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo