Wanawake wadaiwa kutumia mikopo ya halmashauri kuhonga 'viben-10'

Wakati halmshauri nchini zikilalamikia baadhi ya wanufaika kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati, Mkazi wa Butimba jijini Mwanza, Ester Maisoli amefichua kuwa baadhi ya wanawake husindwa kufanya hivyo kutokana kutumia fedha hizo kuhonga vijana "Viben Ten" ili kuongeza upendo.


Maisoli ametoa kauli hiyo leo Februari 16,2023 wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Sh449.7 milioni kwa vikundi 45 vya wanawake, vijana na wenye ulemavu jijini Mwanza ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmshauri hiyo huku akisema baadhi ya wanufaika huanza kufanya matumizi yasiyo na tija ikiwemo kununua nguo, simu za gharama na kufanya starehe 'Kula bata'.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Selemani Sekiete amesema hundi hiyo ya Sh449.7 milioni itanufaisha vikundi 21 vya wanawake, 19 vya, vijana na vikundi vitano vya wenye ulemavu jijini Mwanza.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo