Waziri wa Kilimo Hussein Bashe jana Februari 16, 2023 amekutana na Kufanya mazungumzo na Makatibu watano wa Kanda wa CHADEMA wakiongozwa na Amani Golugwa (Kaskazini), Emanuel Masonga (Kanda ya Kati) Ismail Kangeta ( Magharibi) , Jackson Mnyawami (Serengeti) na Zakaria Obad (Victoria).
Wakati wa mazungumzo hayo ambayo yamefanyika katika Ofisi ya Waziri Bashe Jijini Dodoma, Waziri Bashe amewaeleza Makatibu hao dhamira ya dhati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasasan katika kuleta mapinduzi katika kilimo hasa kubadili maisha ya Vijana wa Tanzania kupitia programu ya Building Better Tomorrow (BBT) ambayo itazinduliwa hivi karibuni.
Makatibu hao wamempa maoni yao kuhusiana na program ya BBT na wao kuahidi kuwa Mabalozi wazuri katika utekelezaji wa programu hyo na wataendelea kutoa maoni huru kwa kadiri ya hatua za utekelezaji zitakavyoendelea.