Mwanafunzi asombwa na maji akivuka mto

Mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Mdete iliyopo mkoani Njombe, Naida Mgaya (12) amesombwa na maji wakati akivuka Mto Makinda huku wenzake watano wakinusurika kufuatia mvua iliyonyesha takribani saa nne mtaa wa Mgendela mjini Njombe.


Akizungumza nasi Mtendaji wa Mtaa wa Mgendela, Agnes Mbilinyi alisema tukio hilo limetokea februari 14,2023 majira ya saa 11 jioni.

"Kama mnavyojua jana kulikua na mvua kubwa sana ndani ya mkoa wetu wa Njombe,hivyo majira ya saa 11 wakati watoto wanatoka shule,shule ya msingi Mdete inahudumia watu wa Mgendela kwa hiyo watoto wanatoka Mgendela wanaenda kusoma Mdete. 

Kwa hiyo wakati wanarudi wakivuka mto maji yalikuwa mengi sana lakini kama mnavyojua changamoto za watoto waliacha kwenda kuvuka kwenye daraja badala yake wakawa wanavuka sehemu ambayo haina daraja"alisema Mbilinyi.

Alisema walikuwa watoto sita lakini mmoja wa kwanza aliyeanza kuvuka ndiye aliyepoteza muelekeo na kutumbukiwa kwenye maji.

"Baada ya kupewa taarifa na wananchi tuliangaika kumtafuta hadi saa sita usiku bila ya mafanikio na tumeamka hii asubuhi na wananchi tupo nao hapa tunaendelea na jitihada za kuendelea kumtafuta mtoto wetu"alisema Mbilinyi.

Akizungumzia tukio hilo, Maua Milinga alisema kuwa wakati yupo ndani alisikia yowe na alivyotoka nje walisikia kwamba kuna mtoto ametumbukia kwenye maji.

"Wale watoto walivyoona mwenzao amevuka mto na kuanza kuelea wakakimbia hadi huku juu ili kusema"alisema Milinga.

Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Njombe, Joel Mwakanyasa, alisema walipokea taarifa kutoka kwa wananchi na kwamba jitihada ya kumtafuta mtoto huyo bado zinaendelea.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo