Kati ya watu 17 waliofariki katika ajali mkoani Tanga, watu 14 ni wa familia moja ambao walikuwa wanasafirisha mwili wa marehemu kwenda mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Ajali hiyo imetokea jana Ijumaa, Februari 3, 2023 majira ya saa 4:30 usiku usiku katika eneo la Magira Gereza Kata ya Magira Gereza Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, barabara ya Segera - Buiko (Barabara Kuu ya Arusha- Kilimanjaro).