Wakazi kutoka Wilaya ya Korogwe na Handeni wamewasili chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe kwa ajili ya kutambua ndugu zao waliofariki kwenye ajali ya gari iliyotokea jana usiku wilayani hapo mkoani Tanga.
Watu hao ambao wengi ni ndugu wenyeji wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, walikuwa wakisafirisha maiti kwenda kwenye mazishi.
Watu 17 wamefariki dunia na 12 kujeruhiwa katika ajali hiyo ambayo imehusisha gari aina ya Coaster lililogongana na Fuso.