Majina 14 ya wanafamilia waliofariki ajalini wakisafirisha msiba

 
Majina ya watu 14 wa familia moja waliofariki katika ajali iliyotokea jana Ijumaa usiku wilayani Korogwe mkoani Tanga yametajwa huku wengine 12 wakijeruhiwa.


Idadi hiyo ni miongoni mwa watu 17 waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Magira Gereza Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, barabara ya Segera - Buiko.



Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Salma Sued imetaja majina ya wanafamilia hao wakiwamo watoto wawili.


“Waliofariki ni Atanasi Rajabu Mrema, Nestory Atanasi, Augustino Atanasi, Kenned Mrema, Godwin Mrema, Yusuph Saimon, Zawadi Mrema, Elizabeth Mrema, Julieth Mrema, Suzana, Rozina  A Lamosa, Evelina Cosmas Mrema na watoto wawili (mtoto wa binamu na mtoto wa Julieth),” amesema Dk Patrick.


Ajali hiyo imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 12.


Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar kwenda Moshi kwenye mazishi ambapo chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva Fuso.


Chanzo:Mwananchi Digital


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo