Uongo wamtokea puani Mkandarasi Makete, Hakutaka Kuchelewesha mambo

Mkandarasi aliyefahamika kwa majina ya Hans Bariki Makenya mmiliki wa Kampuni ya Lucky Construction Limited ya mkoani Dar Es Salaam amefikishwa Mahakamani na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Makete kwa kesi ya kutumia nyaraka za kumdanganya mwajiri ambaye ni Halmashauri ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe kinyume na Kifungu cha 22 cha sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.


Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Makete Chilomwa Bitulo amesema Mtuhumiwa huyo aliandaa nyaraka ya uongo kuwa amejenga Tenki la mradi wa Maji Matamba lenye ukubwa wa ujazo QMita 100 ilihali amejenga QMita 72.5 na kuomba kulipwa fedha za Qmita 100 kinyume na sheria.

Taasisi hiyo imemfikisha Mahakamani mtuhumiwa ambaye alikiri kutenda kosa hilo na Ivan Msaki Hakimu wa Mahakama ya Wilaya hiyo akisoma hukumu, amesema baada ya Mtuhumiwa kukiri kosa anahukumiwa kwenda Jela miaka miwili au Kulipa Faini ya Shilingi Milioni 1.

Mtuhumiwa alikubali kulipa Faini na kuachiwa huru ambapo hata hivyo fedha alizoombaa kulipwa hakufanikiwa kulipwa baada ya kosa lake kugundulika mapema.

Kesi hiyo ilifikishwa Mahakamani hapo Februari 6, 2023 na Hukumu yake kusomwa Februari 7, 2023.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo