Zaidi ya asilimia 96 ya Wanafunzi Makete wameripoti Kidato cha Kwanza 2023

Zaidi ya asilimia 96 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza katika shule mbalimbali Wilayani Makete mkoani Njombe, wameripoti shuleni huku ikielezwa wanafunzi 103 pekee ndio ambao hawajaripoti mpaka sasa.


Akizungumza na Wanafunzi wa Kidato cha kwanza shule ya Sekondari Iwawa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe amesema Kati ya Wanafunzi 2,408 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza ni wanafunzi 103 tu ndio hawajaripoti katika shule zote za Sekondari Wilayani Makete.

Katika shule ya Sekondari Iwawa waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza ni 275 sawa na 100% na tayari wameshaanza Masomo yao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By Peruzibongo