Unyama! Amuua mama yake na dada wa kazi kisa penzi, naye auawa

Tukio la kinyama limetokea jana Jumamosi, Januari 4, 2023, katika eneo la Magomeni Kagera, Mtaa wa Ludewa jijini Dar es Salaam baada ya kijana aitwaye Erick (33) kudaiwa kumuua binti wa kazi wa nyumbani kwao aitwaye Anna (28) kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumkatalia mahusiano ya kimapenzi.


Inaelezwa kuwa,siku ya tukio, mama mwenye nyumba aliondoka nyumbani saa 11 alfajiri na kumuacha mtoto wake wa kiume (Erick) pamoja na msichana huyo wa kazi (Anna) ambaye alikuwa mfanyakazi wake kwa zaidi ya miaka 10 na kufanya kama mtoto wake wakumzaa.

Tukio hilo lidaiwa kutokea asubuhi ambapo kijana huyo baada ya kunyimwa penzi na binti huyo alifunga milango na mageti yote kisha kuanza kumshambulia binti huyo kwa kumchona na kisu kisha kumuua na mwili wake kuutupa chooni.

Majirani wa mtaa huo wamedai walisikia kelele za Anna lakini walishindwa kumuokoa kwa kuwa kijana huyo alifunga mageti yote pamoja na milango na makabati kuyaweka milangoni na kujifungia ndani ambapo kila aliyetaka kuingia ndani alimshambulia kwa kisu.

Muda mfupi baadaye mama yake alifika nyumbani na kukuta damu zimetapakaa kila sehemu ya nyumba, alipojaribu kumuuliza qlipo binti wa kazi, Erick alimshambulia mama yake na kumchoma kisu tumboni kilichopelekea kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

Kelele za mama mtu kuchomwa kisu ziliwashtua majirani ambao walifika eneo la tukio na kuanza kumshambulia mtuhumiwa (Erick) hadi kusababisha kifo chake papo hapo.

Majirani hao wamedai kuwa, binti huyo alikuwa anatishiwa kubakwa mara kwa mara na kijana huyo ambaye akili zake zinadaiwa hazikuwa sawa.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema taarifa hizo za mauaji ni za kweli, tukio limetokea na kinachoendelea ni kuchunguza kwa kina kipi hasa kimesababisha mauaji hayo kutokea kisha watatoa tamko.

“Tunaendelea kuchunguza tukio husika, hatuwezi kuweka wazi hasa kilichotokea, kuna maswali ya kujiuliza huyo kijana aliyeanza kufanya tukio hilo rekodi zake zipoje? Ni mzima? Anasoma? Anafanya shuhughuli gani? Yote hayo ni mambo ya msingi kujua,” amesema Muliro.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo