Simbachawene: Halmashauri yenye njaa iandike barua

Halmashauri ambayo inakabiliwa na tatizo la njaa na kuhitaji chakula imetakiwa kuandika barua kwa Waziri Mkuu kupitia Wizara ya Sera, Bunge na Uratibu ambao ndiyo wenye jukumu la kutoa kibali kwa wataalamu kujiridhisha kama kweli kuna uhitaji wa chakula.


Hayo yamesemwa leo Februari 3, 2023 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Bunge, George Simbachawene wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Ferister Njawu.


Njawu alihoji ni mkakati gani ambao Serikali inachukua katika kuwasaidia Watanzania katika maeneo mengi ambako wanakabiliwa na baa la njaa kwa sasa.


Akijibu Swahili hilo Simbachawene amesema Ofisi ya Waziri Mkuu ikishapokea taarifa ya halmashauri yenye njaa, itaagiza wataalamu kutoka wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambao watakwenda kujiridhisha kama eneo hilo linahitaji chakula cha bei ndogo atatafutwa wakala na kama kunahitajika chakula cha bure taarifa itaeleza.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo