Serikali yaingilia kati mwalimu aliyewapiga wanafunzi kwenye nyayo za miguu

Serikali imeingilia kati sakata la mwalimu aliyeonekana kwenye kipande cha video akiwachapa wanafunzi fimbo za miguuni wakiwa wamevua viatu.


Kipande hicho cha video kimeibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wanahusisha tukio hilo na ukiukaji wa haki za binadamu hasa kwa watoto.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalumu, Dk Doroth Gwajima amewataka wananchi kutoa taarifa wanapoona matukio kama hayo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

"Unapoona vitendo vya ukatili, tuma ujumbe kwenye DM au kwenda namba 0734124191 ili tuweze kushirikiana dhidi ya vitendo hivi.

"Tunaomba taarifa zaidi kuweza kujua ni shule gani na mkoa gani. Asanteni nyote kwa kuendelea kuibua vitendo vya kikatili dhidi ya watoto," ameandika Waziri Gwajima katika ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo, Waziri huyo baadaye aliandika kwamba: "Nimepata tips kuwa ni shule ya msingi iliopo wilaya ya Kyerwa - Kagera na tukio ni la Januari 10, 2023. Mkuu wa mkoa, Albert Chalamila, kesho atatoa taarifa yake. Tusubirie. Situation is under control (jambo linashughulikiwa)," ameandika Gwajima.

Kipande cha video hiyo ya sekunde 43 kinamwonesha mwalimu huyo akiwakanyaga miguuni huku akiwachapa na wanafunzi hao wanasikika wakilia wakimwomba msamaha.

Pia, wizara ya elimu, sayansi na teknolojia nayo inafuatilia suala hilo pamoja na Serikali ya Mkoa wa Kagera.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo