Mwalimu afariki dunia akishangilia Matokeo

Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Musoma Ufundi iliyopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara Gaudence Aloyce (33), amefariki dunia kwa kugongwa na gari muda mfupi baada ya kumaliza sherehe ya kupongezana na walimu wenzake kufuatia shule yao kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne 2022.


Mwalimu huyo pamoja na walimu wenzake walikutana kupongezana baada ya shule yao kupata ufaulu wa 1.7 (GPA) kwenye matokeo yaliyotangazwa na Baraza la mitihani hivi karibuni.

Mkuu wa shule, Magita Nyangore amesema Aloyce alifariki Januari 29, 2023 kwenye barabara ya Nyerere eneo la Baruti mjini Msoma wakati akirudi nyumbani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By Peruzibongo