NJOMBE
Mwenyekiti wa chama Cha demokrasia na maendeleo CHADEMA nchini Freeman Mbowe amewatoa hofu watanzania na Kisha kupongeza mwenendo mpya wa jeshi la Polisi
kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi ya ulinzi wa wananchi na Mali zao katika mikutano ya chama hicho na kisha kudai kwamba chama Chao hakiwezi kuwa chanzo Cha migogoro na uvunjifu wa amani Kama kinavyozungumzwa kwasababu katika mikutano yao hata nzi hauwawi.

Katika mkutano wa chama hicho mkoani Njombe Mbowe amesema wamekusudia kubadili mfumo wa Utawala wa nchi endapo watapata baraka za watanzania kushika dola huku akisema kusudia lao ni kuunda serikali ya majimbo ambayo tayari imeanza kutekelezwa na chama hicho Lengo likiwa ni kuwapunguzia nguvu viongozi kuamua kila kitu Cha wananchi.
Katika hatua nyingine amesema endapo CHADEMA kitashika dola watahakikisha Zao la parachichi linalozalishwa kwa wingi Njombe linapata soko la uhakika na la moja kwa moja.
Mwanzoni mjumbe wa kamati kuu John Heche ameeleza kiu ya chama hicho ya kufanya uwekezaji mkubwa katika migodi ya chuma na mkaa wa Mawe Ludewa kwa kuleta wawekezaji wa viwanda vya kuchakata chuma ili kiweze kunufaisha wakazi wa mkoa huo
Kuhusu mkakati wa kuendeleza sekta ya kilimo mkoa wa Njombe Regnado Danda Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Njombe anasema kulingana na umuhimu wa sekta ya kilimo wataendelea kupambania wakulima kuhusu pembejeo,miundombinu ya Barabara ili malighafi zipelekwe sokoni kiurahisi na kunufaisha Wananchi.