Matetemeko mawili ya ardhi yakiwa na ukubwa wa 4.3 na 4.9 katika kipimo cha Richter, yameikumba mikoa ya Singida na Dodoma ambapo kupitia taarifa kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini nchini (GST) imebainisha kuwa, matetemeko hayo yametokea Februari 16, 2023 na Februari 17, 2023, kwa nyakati tofauti katika maeneo ya mikoa hiyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa,hakuna madhara yaliyoripotiwa kutokana na tetemeko hilo.