Kiongozi wa Upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu amesema kuwa yeye pamoja na viongozi wengine wa upinzani walipumua baada ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufariki dunia.
Lissu ambaye alirejea Tanzania hivi karibuni baada ya miaka kadhaa nchini Ubelgiji alipokuwa akizungumza wakati wa mahojiano ya moja kwa moja na Clouds TV Ijumaa, 3 Februari 2023, ambapo alifichua kuwa ilikuwa ahueni kubwa kwao kwa upinzani wakati Magufuli alipoaga dunia.
Kwa mujibu wake, Magufuli alikuwa kiongozi mbovu aliyewadhulumu viongozi wengine walioipinga serikali yake na uongozi wake, na kuongeza kuwa hawezi kujifanya na kumzungumzia Magufuli kwa nia njema kama viongozi wengine wamekuwa wakifanya.
"Kuna watu wanasema marehemu hazungumzwi kwa mabaya, nauliza hivi Idd Amin baada ya kufa anasemwa kwa uzuri upi, Mtu mwovu akifa watu wanapata ahueni, kifo cha Magufuli kilitupa afueni maana alitutesa sana na wanaodhani hakuna afueni ni wale waliokuwa wananufaidika naye," Alisema Tindu.
Wanamitandao walitoa hisia tofauti huku wakimlani Tundu kwa matamshi yake.
rushunjufrido: Una laana siyo Bure we waona mabaya tu hakuna mazuri alifanya chuki zako binafsi hazitakusaidia zaidi ya kuendelea kujishusha thamani Mpuuzi tu mmoja
johnyusuph711: Acha zako wewe, ahueni umepeta wewe na tofauti zenu sisi wengine tulimhitaji.
mustafamulimbo: We tetea ugali wako muze ila muto unakusubiri mbiguni????
andrewpius72: Nadhani ni Upumbavu zaidi, kuliko umuhimu wa jambo lenyewe, ukikosa hoja ni bora kutulia kuliko kuacha kutulia na watu wakajua Upumbavu wako. Macho yanaona kama miwani haioni vzr kilichofanyika.
izbet_shija: Ahueni ya wasio julikana labda. Ila maisha magumu ni pale pale
fficialaine3: Ila huyu licha Mungu kumnusuru na kifo bado anamuongelea vibaya Magufuli,utasema yeye atabaki tena milele! Na akimaliza tena miaka miwili hapa Tanzania nimekaa pale.
Chanzo:BBC