DC mpya Mbogwe akabidhiwa ofisi, Ni baada ya wa Awali Kuingia mitini

 
Mkuu mpya wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kuwa mkuu wa Wilaya hiyo ili aweze kuwatumikia Wananchi.


Katika taarifa iliyowekwa na Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magesa Jumapili kwenye kundi la WhatsApp la waandishi wa habari na viongozi wa mkoa huo imeeleza makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba aliyekua akikaimu nafasi hiyo, amesema ni heshima kwake kuaminiwa na kuahidi kutumika kwa maendeleo ya wananchi wa Mbogwe.

Sakina amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya hiyo pamoja na wakuu wa vitengo vya halmashauri kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake Ili kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.

Mkuu huyo mpya wa wilaya ya Mbogwe aliapishwa Februari 15, 2023 katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wakiwemo wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa CCM.

Uteuzi wa Sakina umefanyika kuziba nafasi ya Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Leah Ulaya aliyeteuliwa awali kuwa mkuu wa wilaya hiyo kutoripoti kazini.
Chanzo: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo