‘Msiogope kuwatania polisi’ yamuibua SACP Misime

Jeshi la Polisi limekemea vikali kauli zinazosambazwa kwenye mitandao zenye nia kupotosha na kuwaambia kuwa taasisi hiyo imeundwa kwa mujibu wa sheria si kwa ajili ya kufanya utani bali kutekeleza majukumu mahususi ambayo ni kulinda maisha ya watu na mali zao.


Taarifa iliyotolewa leo Februari 18, 2023 na Msemaji wa Jeshi Polisi, SACP David Misime imeeleza kwamba taarifa iliyosambaa jana kuhusu utani hailihusu jeshi hilo.

“Jeshi la Polisi ni taasisi iliyoundwa kwa mujibu wa sheria si kwa ajili ya kufanya utani, bali kutekeleza majukumu mahususi ambayo ni kulinda maisha ya watu na mali zao, kulinda amani na utulivu.

Kusimamia utekelezaji wa sheria, kubaini na kuzuia uhalifu, kukamata wahalifu na kupeleleza kesi,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

“Tunaomba ieleweke kauli hiyo haikutolewa na Jeshi la Polisi na hatuna utani katika kutekeleza majukumu tuliyopewa kwa mjibu wa sheria,” imeeleza taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP Misime na kuongeza,

“Tunachoendelea kuomba kutoka kwa wananchi ni ushirikiano katika kubaini na kuzuia uhalifu na siyo utani kama huyo aliyeamua kuupotosha umma,” imefafanua taarifa hiyo.

Jana kwenye mitandao ya kijamii kulisambaa ujumbe uliokaririwa ukisomeka ‘Msiogope kuwatania Polisi’.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo