Baba wa kambo na mama mzazi watuhumiwa kuua mtoto mdogo


Mtoto wa miaka 6 Paul Haule ameuawa na kufukiwa kwenye shimo la takataka ambalo lipo karibu na nyumba yao ambapo tukio hilo limetokea katika kijiji cha Peramiho A kata ya Peramiho wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.


Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linawashikilia baba wa kambo wa mtoto huyo pamoja na mama mzazi wa mtoto kwa tuhuma za kufanya mauaji ya mtoto huyo.

Wakiongea baada ya tukio hilo kutokea baadhi ya majirani ambao walishuhudia tukio hilo, wanasema mtoto Paul Haule ambaye ana umri wa miaka 6 alipotea katika mazingira ya kutatanisha ambapo wananchi wa kijiji cha Peramiho A kwa kushirikia na jeshi la polisi mkoani Ruvuma walifanya jitihada za kumtafuta mtoto huyo mpaka walipofika katika nyumba ambayo mtoto huyo anaishi na kufukua shimo la takataka ambalo lipo katika nyumba hiyo na kumkuta mtoto huyo amefukiwa na ameshafariki.

Kwa upande wake Nichorus Nganemanu diwani wa kata ya Peramiho anaelezea hatua ambazo serikali ya kata ya Peramiho ilizichukua baada ya kupata taarifa ya mtoto huyo kupotea.

Akiongea kwa njia ya simu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma ACP Marco Chilya amesema jeshi hilo linawashikilia baba wa kambo wa mtoto pamoja na mama mzazi wa mtoto kwa tuhuma za kufanya mauaji ya mtoto huyo huku chanzo kikiwa ni imani za kishirikina.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo