Aliyeua mtu kwa kumchoma visu aachiwa huru

Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora imemuachia huru Jonas Charles maarufu Mkondo Abisai, mkazi wa WIlaya ya Sikonge aliyekuwa akikabiliwa na makosa ya kuua bila kukusudia. 


Jonas alishitakiwa kumuua bila kukusudia kwa kumchoma kisu mara tatu Willson Kaswiza mwaka 2010.


Akisoma uamuzi huo wa mahakama, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Dkt. Mwajuma Kadilu Juma alisema mahakama imepitia hoja za pande zote mbili katika shauri hilo na kubaini kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo bila kukusudia.

Na kwa kuwa ameshakaa muda wa zaidi ya miaka sita gerezani ambao unatosha kuwa adhabu, hivyo ameachiwa huru huku akitakiwa kwenda kuishi kistaarabu na jamii pasipo kutenda makosa ya aina hiyo.

Awali upande wa mashtaka chini ya wakili Tunosye Luketa uliiambia mahakama kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 22 mwaka 2010 baada ya kumchoma kisu zaidi ya mara tatu marehemu Willson katika vurugu zilizotokea wakati wakiwa kwenye moja ya starehe Kijiji cha Kawale, wilayani Sikonge.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo