Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkoano wa Chama cha CCM juzi
alinusurika kupigwa na wananchi wa tarafa ya Kiagata baada ya kuonekana
akifanya kampeni na kuhamasisha wananchi kuchagua chama chake.
Kitendo hicho cha mkono kuonekana akifanya mazungumzo na vikundi vya
watu mbalimbali waliokua maeneo ya kupigia kura kulifanya wananchi
kuanza kumhoji kama muda huo ni wa kampeni ama kupigakura.
Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya wananchi kuzidi kumsonga kitendo
kilichofanya ashindwe kujitetea kutokana na umati wa wananchi ambao
walianza kumzomea.
Mwenyekiti mstaa wa kijiji cha Sirori Simba Alexender alisema Mkono
alifika eneo hilo akiwa na gari lake na kuanza kuzungumza na wananchi
katika vikundi mbalimbali hali iliyofanya watu kuanza kumnung’unikia na
kudhani amekuja kwa nia ya kufanya kampeni.
