Aliyekuwa anazikwa ajitokeza Mazishini hapo akiwa Mlevi, Waombolezaji watimua mbio

Kizaazaa kilishuhudiwa katika kijiji cha Itakaibolu mkoani Kaliro nchini Uganda baada ya mwanamume ambaye alistahili kuwa anazikwa kujitokeza katika mazishi yake akitembea.


Katika kisa hicho kilichotokea mnamo Jumanne - Februari 7 - Asadi Ndekeire alifika kwenye hafla ya akiwa mlevi pamoja na rafiki zake ambao pia walikuwa wamebungia mvinyo. Hali hii iliishtua familia pamoja na waombolezaji. Nini haswa kilitokea? Inaarifiwa kuwa Ndekeire ambaye anajulikana kijijini humo kama mraibu hatari wa pombe, aliwasili katika hafla hiyo pamoja na rafiki wake wote wakiwa wamelewa na kuketi viti vya nyuma.


Lakini jeneza liliposhushwa kaburini, Ndekeire pamoja na rafiki zake walitembea kwa ulevi wao hadi kando na kaburi kumuaga mwendazake kwa kurusha udongo kaburini. "Alikuwa mwanamume mzuri ambaye alimfanya kila mtu kucheka. Lakini nyumbani alikuwa mwanamume mdhoofu ambaye alikuwa akilia kila saa kama mtoto kwa sababu mke wake alikuwa akimponda kama mhogo wa kitamaduni," Ndekeire amenukuliwa na gazeti la Daily Monitor. Waombolezaji wakimbia kwa hofu Kizaazaa kilizuka baada ya waombolezaji kutambua sauti hiyo. 


Kila mtu aligeuka kuangalia walichokuwa wakidhania kuwa ndicho. Mwanamke mmoja aliyetambua hilo wa kwanza alipiga kamsa na kila mtu kukimba kwa hofu akiwemo Ndekeire. Kundi la wanaume lilimfukuzia na kumshika Ndekeire kisha kumrejesha nyumbani familia yake ikisema kuwa alikuwa hajaonekana kwa siku kadhaa jambo ambalo si kawaida kwake.


 Mwanamume mmoja alipopatikana akiwa amefariki kwa kugonga na lori katika baa ya karibu ambapo Ndekeire ni mteja wa kila mara alidhaniwa kuwa yeye kwani mwili na uso vilikuwa vimeharibika vibaya.


Ila kwa kuelezea chanzo cha yeye kutoweka kwa siku hizo zote, mwanamume huyo alisema kuwa alikuwa ametekwa nyara na watu ambao wanamdai pesa zao.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo