Nyuki wamuua mwalimu

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mambo iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma Deogratius Emili Ndokoye (51) amefariki papohapo baada ya kushambuliwa na kundi la nyuki waliokuwa kwenye mti wa mwembe maeneo ya nyumbani kwake Mtaa wa Masanga.


Nyuki hao walimvamia Mwalimu huyo muda mfupi baada ya Watoto waliokuwa wakitoka Shuleni kutupa mawe juu ya mwembe huo na kusababisha nyuki kuanza kuzagaa ndipo walipomvamia na kuanza kumshambulia hali ambayo ilisababisha kupoteza maisha.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Masanga, Lubabi Aron Nyabakali amesema tukio hilo sio la kwanza katika eneo hilo, mara ya kwanza nyuki hao walivamia mifugo ambapo mbwa wawili walikufa na kuziomba Mamlaka za Maliasili kufanya harakati za kuwatoa nyuki hao na ikibidi mwembe huo ukatwe kwa ajili ya usalama wa wananchi.

Majirani wamesema walifanya jitihada za kuyaokoa maisha yake lakini hawakufanikiwa kwakuwa nyuki walikuwa wengi na wakashindwa namna ya kuwadhibiti kwa uharaka zaidi.

Marehemu mwalimu Deogratius amecha Mke na Watoto watatu, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Nyabitaka tarafa ya Mabamba iliyopo Wilayani Kibondo kwaajili ya hatua nyingine za mazishi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo