Ajifungua mapacha watano, Wote wafariki Dunia

Furaha imegeuka kilio kwa familia ya Nakuru iliyobarikiwa na watoto watano katika hospitali ya kaunti ya Nakuru baada ya kifo kubisha hodi.


Watoto hao watanano, wasichana wanne na mvulana mmoja, wameripotiwa kufariki dunia ikiwa ni masaa chache tu baada ya kuzaliwa. 


Daktari mkuu katika hospitali hiyo Aisha Maina amesema watoto hao walifariki dunia Alhamisi Februari 2, 2023 


Mbunge wa Bahati Irene Njoki ni miongoni mwa wale ambao wamefikisha rambirambi kwa familia hiyo.


"Mambo yameisha vibaya, malaika hao watano walale pema," aliandika Njoki kupitia ukurasa wake wa mtandao. Wakenya walikuwa wamepokea taarifa za baraka hizo zilizobisha kwa Simon Ndung'u na mkewe Margaret Wangui. 


Wangui alifika kwenye hospitali hiyo ya PGH na kujifungua watoto hao watano jambo ambalo liliipata familia yake kwa mshangao. 


Alisema hakuwa ametarajia kupata watoto hao kwani ukaguzi wakati wa kliniki ulikuwa umeonyesha ana watoto watatau.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo