Siku moja kabla ya siku ya wapendanao yaani Februari 14, 2023 Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema itakuwa ni mwisho wa matumizi ya laini ya simu ambayo haijahakikiwa
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma leo Januari 24,2023 Waziri Nape amesema kwa sasa tarehe ya mwisho ya kuhakiki ilikuwa Januari 31,2023 lakini serikali imeongeza siku 14 ambapo mwisho utakuwa tarehe Februari 13,2023 na hakuna muda utakaoongezwa tena baada ya hapo ambapo muda wa kuzizima ni saa kumia kamili jioni
Amesema kila mtu anatakiwa kuhakiki laini zake zote za simu na endepo kuna laini haitahakikiwa basi itafungwa na haitatumika tena
Waziri Nape amesema laini zilizosajiliwa ni hadi kufikia Januari 19, 2023 ni 60,739,790 ambapo kati ya hizo laini zilizohakikiwa mpaka tarehe hiyo ni 58, 432, 639 na ambazo bado ni 2, 307,151.
Amewaonya waandishi wa habari nchini kuacha kuwatetea wezi (wahalifu) hasa katika suala hili la uhakiki wa laini za simu.