Simbachawene awasihi Watanzania kuiombea nchi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene, ameomba wananchi kuendelea kuiombea nchi dhidi ya majanga mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukame, njaa, mafuriko na ajali.


Kauli hiyo ameitoa kwenye mkesha wa kitaifa wa dua maalum kwa taifa la Tanzania ambao umetumika kuuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam tarehe 31/12/2022.


"Tumuombe Mungu kwa mwaka 2023, ili tuendelee kuenzi na kudumisha tunu za Taifa letu za amani, umoja, mshikamano, utu, haki, heshima ya mwanadamu, uhuru na demokrasia," amesema Waziri Simbachawene


Waziri Simbachawene amehimiza kuendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi, watu wake na usalama wa mali zao, ikiwa ni pamoja na kuwa na serikali madhubuti, inayosikiliza na kutekeleza matakwa ya wananchi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.


"Tuwaombee viongozi wetu wakuu, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar afya njema na nguvu ya kutosha kuendelea kuisimamia miradi ya kimkakati kwa ufanisi kama ilivyokuwa kwa mwaka 2022 ili iweze kukamilika katika wakati uliopangwa," ameongeza Simbachawene


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo