Pasta mmoja nchini Nigeria amezindua chupi na sindiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake waseja wanaotamani kuolewa kuwavizia waume zao.
Kulingana na pasta Dr J.S. Yusuf, ambaye ni mkuu wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja, aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za 'baraka' ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.
Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema “Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.” Pia alisema kuwa chupi hizo zinapovaliwa na wanawake, zitawasaidia kupigana na magonjwa na kupata bahati njema ya kuwavizia wanaume ambao watawaoa.