Mwanamke mmoja amesimulia kisa cha swahiba wake ambaye alivunjika moyo baada ya kugundua kuwa mume wake ambaye wamekuwa pamoja katika ndoa kwa miaka saba ni shoga.
Mfanyabiashara wa Nigeria, Valencia Poise, kupitia ukurasa wake wa Instagram, alisimulia namna rafiki yake mwenye umri wa miaka 46, aligundua kuwa mumewe alikuwa shoga baada ya miaka saba ya ndoa bila kushiriki ngono.
Mfanyabiashara wa Nigeria, Valencia Poise, kupitia ukurasa wake wa Instagram, alisimulia namna rafiki yake mwenye umri wa miaka 46, aligundua kuwa mumewe alikuwa shoga baada ya miaka saba ya ndoa bila kushiriki ngono.
Wakati walipokuwa wakichumbiana kwa miezi mitatu, mume wake alimuomba wasijamiane akidai kuwa Mkristo mzuri na alifurahishwa na msimamo huo kwani kwa wengi unatafsiriwa kuwa 'mtu mwema'.
Lakini walipooana, mwanamume huyo alisingizia kwamba alikuwa na shida ya kiuno hivyo kumfanya mkewe kusubiri zaidi kupakuliwa asali. "Mwanamke huyo alimngoja mume wake kwa uaminifu hadi alipomuoa kitamaduni na kanisani baada ya miezi 3 ya uchumba. Utafikiri angelishiriki tendo la ndoa lakini hakufanya hivyo, alimdanganya kuwa alipata ajali miezi michache nyuma ambayo iliathiri kiuno chake na bado alikuwa akipona kutokana na upasuaji huo."
Lakini mrembo huyo alianza safari nyingine mpya ya kusubiri na wakati ngoja ngoja yake ilipoanza kumuumia matumbo, mume wake alimpeleka kwa daktari fek ili kumtuliza. Daktari huyo feki alimhakikishia mwanamke huyo kuwa kila kitu kilikuwa shwari na kwamba mumewe alihitaji muda zaidi kupona kabisa kabla ya kutekeleza majukumu yake ya chumbani.
"Akitokea kwa daktari, utafikiri ni kweli kumbe ulikuwa ni mpango kati ya mumewe na daktari kumdanganya. Aliendelea kusubiri majeraha ya kiuno yapone," aliongeza.
Baada ya miaka 3 na nusu ya kusubiri majeraha ya kiuno yapone, mumewe alirejea nyumbani siku moja na akiwa amemnunulia vya ngono na kumwambia kuwa alihisi amemvumilia sana, hivyo alimtaka kuvitumia kujitosheleza haja yake. Vile vile alimruhusu kuenda nje ya ndoa na kuchumbiana na mwanamume yeyote e ila sharti kuwa asiwahi kumjua mwanaume anayemtosheleza kingono.
Lakini mbio za sakafuni za mumewe wake zilitimia mnamo Juni 2022, baada ya kumfumania mume wake akirushana roho na mwanamume mwenzake kitandani.