Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Songwe kuhakikisha linawasaka na kuwakamata watu waliohusika katika tukio la mauaji ya mfanyakazi wa TANESCO aitwaye Angel Shakinyau (33) aliyeuawa usiku wa kuamkia Januari 16, 2022 na mwili wake kutupwa jirani na nyumba anayoishi.
Marehemu Angel Shakinyau anadaiwa kuvamiwa usiku wakati akirudi nyumbani kwake na kisha kuuawa kwa kunyongwa na kamba inayodaiwa kuchanwa kwenye turubai ya Bajaji.
Mwili wa marehemu umeagwa katika makazi yake mjini vwawa na kusafirishwa kwenda mkoani Dodoma Kisha kwao Shinyanga kwa ajili ya mazishi.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amewahasa watu wote ambao wanafanya vitendo vya ukatili ndani ya Songwe hawatakuwa salama tena, kwani watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za Nchi.