skip to main |
skip to sidebar
PICHA NA HABARI KAMILI YA KUUNGUA KWA MARA YA PILI MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI
Msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Saam uliungua
kwa mara ya pili leo. Msikiti huo ambao uliungua mnamo Agosti 13,
2014 katika ghorofa yake ya juu na kuteketeza eneo kubwa ambalo hadi
sasa bado halijanza kufanyiwa ukarabati.
Leo hii
moto ambao inasemekana ulianza mmajira ya saa sita na nusu
mchana katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kidato cha nne wa
kike wamekuwa wakipiga kambi ya kujisomea ikiwa ni katika maandalizi ya
kukabiliana na mtihani wao wa taifa utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Kanda ya Kinondoni Camilius Wambura amethibitisha
jambo hilo na kusema kuwa hadi wanafika eneo la tukio chanzo bado
hakijafahamika, na kwamba chumba ambacho moto ulianzia ni cha wasichana
ambamo magodoro manne yameungua.
“Katika janga la
moto uliounguza madarasa mwezi uliopita Jeshi la Polisi iliunda timu
ambayo ilikuwa ikichunguza chanzo cha moto huo hivyo na sasa timu
hiyohiyo itaendele na uchunguzi wake kwa kuunganisha matukio haya
mawili” alisema Wambura.
Wakizungumza bila ya
kutaja majina yao kina mama wa msikitini hapo wao walisema kwamba “
sisi tulikuwa msikitini tunasoma qurani wakati tukivuta muda wa sala ya
Ijumaa ndipo tuikasikia sauti za moto moto na kuona upande wa wanaume
wakikimbia huku na kule kwa taharuki hivyo chanzo hasa cha moto sisi
hatukijui.
Waumini wa msikiti huo walifanikiwa kuuzima moto huo na kusali swala ya Ijumaa kama kawaida. 
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi