Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt Fredrick Shoo amesema suala la kupewa likizo ya siku 60 na kuondolewa kwenye Usharika wa Kijitonyama Mchungaji wa Usharika huo Dkt. Eliona Kimaro ameliona mtandaoni na kukiri kwamba uamuzi huo umefanyika katika ngazi ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani
Dkt Shoo amesema taarifa hizo bado hazijatumwa kwake rasmi na amewaomba waumini kuendelea kuwa watulivu, "Niombe utulivu kwa washarika na wakristo ambao wamesikia habari hizo za uamuzi ambao umefikiwa na dayosisi yake, tambua kwamba dayosisi ina vyombo vyake vya maamuzi na bila shaka jambo lenyewe linaendelea kufanyiwa kazi na dayosisi husika"
TAZAMA SAKATA HILO HAPA CHINI